Na mwandishi wetu
Benchi la Ufundi Yanga limeeleza kufurahishwa kwake na ratiba ya Ligi Kuu ya NBC iliyotolewa jana na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kwa madai kuwa imekaa katika mkakati wao waliojiwekea kuelekea msimu ujao.
Kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kwamba ratiba hiyo imekuwa kama ni faida kwao kwa kuwa wanaanza na timu ambazo zimekuwa zikiwasumbua hivyo ni vyema wakamalizana nazo mapema.
Katika ratiba hiyo, Yanga itaanza kampeni ya kutetea taji hilo kwa kucheza na Polisi Tanzania Uwanja
wa Ushirika, Moshi na baada ya hapo itacheza na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kisha itarejea Dar es Salaam kuumana na Azam FC.
“Mechi hizo tatu ni kama fainali na dira kuelekea mbio za kutetea taji letu la Ligi Kuu, msimu uliopita timu zote tatu tulizifunga kwenye mechi zote mbili za ligi na Coastal tulicheza nao mara tatu zaidi ikiwemo mchezo wa fainali ya Kombe la FA, ni wazi hawatokubali kuendelea kupoteza dhidi yetu,” alisema Kaze.
Kocha huyo ameeleza kuwa pamoja na yote wamekiandaa kikosi chao kikamilifu kuhakikisha kinakabiliana na changamoto yoyote itakayojitokeza kwenye ligi sababu bado wana malengo ya kuendelea kutawala soka la Tanzania.
Kaze alisema wanachojivunia ni usajili mzuri ambao wameufanya kwenye dirisha kubwa na idadi kubwa ya wachezaji wao kukaa pamoja kwa muda mrefu, kitu ambacho hakijapoteza muunganiko wa timu yao.
Soka Kaze: Ratiba nzuri kwa Yanga
Kaze: Ratiba nzuri kwa Yanga
Read also