Na mwandishi wetu
Kiungo mchezeshaji wa Simba, Larry Bwalya amejinasibu kuwa wanataka
kuweka rekodi na kufuta kushindwa kwa timu za Tanzania kufikia hatua
ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Saa chache baadaye Simba itaingia dimbani kuumana na Orlando Pirates
ya Afrika Kusini kuwania tiketi ya nusu fainali ya michuanKombe la
Shirikisho Afrika.
Mara ya mwisho Simba ilifika fainali ya michuano hiyo wakati huo
ikiitwa Kombe la CAF mwaka 1993 na sasa Simba inataka kurudia rekodi
yake hiyo msimu huu kwa kutinga nusu fainali na kwenda fainali baada
ya kukwama kwenye robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika msimu uliopita.
Bwalya amedai kuwa wanafahamu nini wamekwenda kufanya dhidi ya Orlando
na ingawa wana faida ya ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye mechi ya
awali Jumapili iliyopita lakini bado wana kitu cha kufanya kuhakikisha
wanapita hatua hiyo kwa kishindo.
“Tunajua kwa nini tumekuja kwenye mechi hii ta marudiano, lengo ni
kushindana na kama kocha alivyosema ni muda mrefu tangu timu ya
Tanzania ifike nusu fainali kwa mashindano ya Afrika kwa hiyo kama
timu kama wachezaji mmoja mmoja tunajua hii mechi ina umuhimu kiasi
gani.
“Haitakuwa mechi nyepesi, Orlando wako nyumbani na sisi tuna faida ya
ushindi, hatutakiwi kuitegemea, inabidi tupambane kuhakikisha
tunaingia nusu fainali, hilo ndiyo litakuwa la muhimu zaidi kwa sasa,”
alisema Bwalya anayetumia mguu wa kushoto.
Mechi hiyo itapigwa saa 1.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kwenye
dimba la Orlando, Soweto mjini Johannesburg, mshindi wa matokeo ya
jumla ya mechi hiyo atacheza na mshindi wa mechi ya Al Ittihadi dhidi
ya Al Ahly Tripoli, zote za Libya.
Na Simba itaingia uwanjani hapo ikiwa na mtihani mwingine kuhakikisha
haifanyi makosa dhidi ya timu za Afrika Kusini kama ilivyotokea msimu
uliopita walipong’olewa na Kaizer Chiefs kwa ushindi wa jumla wa mabao
4-3. Simba ilichapwa mabao 4-0 ugenini kabla ya kushinda mabao 3-0
nyumbani.
Mechi nyingine za hatua hiyo zinazopigwa leo ni TP Mazembe
ikiikaribisha Pyramids huku Tripoli ikiwa mwenyeji wa Ittihad. Mechi
zote mbili za awali baina ya timu hizo ziliisha kwa suluhu. Kesho RS
Berkane iliyopoteza ugenini kwa mabao 2-1 dhidi ya Al Masry
itahitimisha ratiba ya hatua hiyo ikiwa nyumbani.
Kimataifa Bwalya: Tunataka rekodi kwa Orlando
Bwalya: Tunataka rekodi kwa Orlando
Read also